Na.Archandramu Mbungu.
Ugonjwa wa taifodi au homa ya matumbo ni ugonjwa unaodhuru viungo( organi) mbalimbali mwilini na huanzia tumboni, ugonjwa huu husababishwa na kimelea aina ya bakiteria anaeitwa salmonella typhi na wakati mwingine salmonella paratyphi
Vimelea hawa wanapokua kwenye tumbo husafiri kwenye mishipa ya damu na kufika sehemu mbalimbali za mwili kama mifupa, ini bandama, na kisha huzaliana kwa wingi ndani ya chembe zinazolinda mwili ziitwazo macrophage kwenye mifupa, Ini, bandama na mitoki.Mara baada ya kuongezeka huharibu chembe hii inayolinda mwili na na kisha kutolewa kwa wingi na huvamia zaidi mwili na kusabaisha dalili mbalimbali
Vimelea hawa wanabebwa na binadamu ambao wanakua hawana dalili zozote za ugonjwa huu na endapo atajisaidia na itakotea kinyesi chake kimechanganyika na maji basi hata maji yanayooshea chakula au kunywa endapo hayajachemshwa vyema mtu anaeza kupata maambukizi hayo
Je kuna vihatarishi vya kupata ugonjwa huu?
Vimelea vya ugonjwa huu havina kiumbe kingine kinachoweza kuvisafilisha isipokuwa binadamu
Njia zifuatazo husafilisha kimelea huyu;
- Kula vyakula na vinywaji vilivyotengenezwa na mtu mwenye taifodi( akiwa haoneshi dalili yoyote au anaonesha dalili) ambaye anasambaza vimelea kupitia kinyesi kama asipozingatia usafi wa kunawa mikono au kwa nadra sana mkojo
- Kutofanya usafi wa mikono( kutonawa mikono baada ya kutoka chooni)
- Kula chakula kilichochanganyika na kinyesi kutokana na mifumo mibaya ya maji taka( maji taka kuelekezwa kwenye maji safi wanayotumia binadamu, kujisaidia kwenye vyanzo vya maji) au magamba ya samaki
Vimelea hawa wa taifodi huweza kuishi hadi kwenye tindikali iliyopo tumboni kwa kuvumilia kidogo na wengine hufa, lakini dawa za kuzuia uzalishaji tindikali tumboni (ant acid) huweza kuongeza kuishi kwa vimelea na kusambaa. Watoto wengi walio shuleni na watoto wadogo wapo hatarini kupata ugonjwa huu na dalili zao huwa hazifanani sana na ugonjwa huu. Wanaweza kupata homa kiasi au kifafa na wakati mwingine hawana dalili zozote mpaka vipimo vifanyike
Zipi ni dalili za ugonjwa wa taifodi?
Dalili za taifodi inayosababishwa na S.typhi na s.paratyphi hazitofautiani sana, hutokea siku 7-14 baada ya kuambukizwa na huwa kama ifuatavyo
- Homa inayoongezeka siku nzima na kupungua asubuhi inayofuata
- Baada ya wiki moja ya ugonjwa huu mabadiliko ya tumboni yanatokea kama
- Maumivu sehemu zote za tumbo na maumivu tumbo likiguswa
- Maumivu ya kuchoma sehemu ya kulia ya juu ya kitovu
- Choo kigumu au kukosa choo kabisa wakati wote wa ugonjwa
- Mgonjwa ndipo anaweza kupata kikohozi kikavu, maumivu kiasi mbele ya kichwa ugonjwa wa kupungua fahamu kutokana na kuharibika kwa ubongo(derilium) na kuchoka sana
Baada ya wiki ya kwanza kuisha,
- joto kupanda na kushuka 39-40 C.
- Mgojwa anaweza kupata mabaka madogo madogo mwilini na kuisha ndani ya siku 2-5.
Baada ya wiki mbili dalili hizo hapo juu huongezeka maradufu
- Tumbo huvimba na kuwa kubwa, bandama kuvimba hutokea maranyingi
- mapigo ya moyo kwenda polepole
Wiki ya tatu mtu anakosa hamu ya kula na mgonjwa anazidi kuwa na hali mbaya zaidi na kupoteza uzito
- Maambukizi kwenye sehemu nyeupe ya jicho(conjuciva hutokea )
- pia mgonjwa anaweza kupata shida ya kupumu, kupumua haraka haraka na pia anakuwa na sauti kwenye mapafu endapo atasikilizwa na dakitari, wakati mwingine mgojwa anapata choo chenye rangi ya kijani na njano , kuharisha na kuchanganyikiwa. Wakati mwingine utumbo unaweza kutobolewa na waudu hawa
Ikiwa mtu amepitia kipindi hiki cha wiki nne bila matibabu, homa, tumbo kuvimba na kutojitambua huweza kupotea polepole lakini wakati mwingine mfumo wa fahamu unaweza kuhalibiwa usijirudie hali ya mwanzo
Vipimo gani vinaweza kufanyika kwa mtu akifika hospitali?
Vipimo mbalimbali vinaweza kufanyika kama
- Kukuza vimelea, huchukuliwa kwenye mifupa na na kuotesha (culture) ambachoo hugundua kimelea huyu kwa asilimia 100. Mkojo na kinyesi maranyingi havitumiki kwa sababu uwezo wa kumtambua kimelea huyu ni mdogo
- Damu inaweza kutumika kufanya kipimo hiki ka kukuza vimelea hivo
- Kipimo cha PCR kinachogundua vinasaba vya kimelea husika
No comments:
Post a Comment