Friday, 2 September 2016

AJIRA KUSITISHWA HADI NOVEMBER 2016

AJIRA KUSITISHWA HADI NOVEMBER 2016

Serikali kupitia kwa waziri S. Jaffo Katika Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Inapenda kuwataarifu wananchi wote kwa Ujumla ususani wale wahitimu wa Vyuo vikuu kwa mwaka 2015/2016  ambao wanasubiri Ajira kutoka Serikalini kua Kutokana na Zoezi la Kuhakiki Watumishi Hewa na Uwepo wa tatizo jipya ambalo ni Wanafunzi hewa , Serikali imetoa maelekezo ili Matatizo hayo yapatiwe Ufumbuzi na Kumalizwa kabisa hivyo Serikali imetoa Muda wa Mwezi mmoja kwa Viongozi wote walioapishwa na Mh. Raisi kuhakikisha kua tatizo linaisha na Kutangazwa kwa ajira mpya Mapema iwezekanavyo.

Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza ikumbukwe lengo la Serikali ni kurekebisha  Kuboresha na kuhakikisha Mazingira ya Watumishi wake yanakua Mazuri kuliko awali ili watumishi hao Wafanye kazi kwa Ari na iwe na Tija.

Ofisi ya Raisi
Kurugenzi ya Mwasiliano
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

No comments:

Post a Comment