MWENYEKITI WA CCM MH DR JOHN MAGUFULI
MAPOKEZI KATIKA OFISI NDOGO YA MAKAO MAKUU YA CCM, LUMUMBA
12 .8.2016
DONDOO
#Ninawashukuru wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM kwa kunipa uwenyekiti wa chama chetu. Huenda sikustahili, lakini walinichagua. Ninwashukuru sana.
#Nitatumia akili zangu na nguvu zangu zote kuwafanyia kazi watanzania kwa bidii.
#Chama cha Mmapinduzi ndio chama tawala...kipimwe ndani ya miaka mitano.
#Tumeamua kufanyakazi. Nataka niwahakikishie watanzania wenzangu...tumepanga kufanya kazi.
#Katika CCM...tumepanga kujisahihisha...
#CCM ilianza kupoteza dira. Chama kilianza kuwa cha matajiri...
#Nimejipanga kufanya kazi kwa kushirikiana na watanzania wote.
#Nataka nijenge chama chenye maadili nazuri kama alivyokiacha Mwalimu Nyerere. Nataka nirudishe heshima ya chama hiki. Ninawaomba wana ccm wenzangu...wakati ninafanya kazi ya kurudishnidhamu ya chama mnivumilie. Maananitakapoamua kunyoosha, nikikunyookea...
#Natakaccm mpya
#CCM imeundwa na wanachama wa kawaida...kamwe sitakubali watu wanaotaka uongozi ndani ya chama watumie pesa...
narudia kusema...
#Yeyote mwenye uwezo wa kuongoza mwakani aombe uongozi. Atakayetumia rushwa ajuehatarudi
#Ninataka ccm mpya. ninataka Tanzania mpya. Twende na kuhakikisha tunaondoa kero za wananchi wetu.
#Ilifikia mahali watoto wa maskini wanarudishwa nyumbani kwa kukosa karo...ndio maana sasa tumeamua kutoa elimu ya sekomdari bure.
#Sasa nataka niwaeleze, msiangaike kunywa vidonge vya majira, zaeni...fyatueni watoto kwasababu watasoma kuanzia la kwanza hadi sekondari.
#Hakuna mtoto atakayerudishwa nyumbani eti kwa kukosa ada, awe CCM, UKAWA, CUF...
#Tutaendelea kusimamia nidhamu ndani ya Serikali
#Mapato: Makusanyo yamapato yameongezeka.
#Nataka niwahakikishie, tumejipanga kufanya kazi kwa niaba yamaskini wa nchi yetu. Mimi mwenyewe ni mtoto wamaskini.
#Ninataka tujenge nidhamu ndani yaSerikali
#Tupo kwa ajili ya watu wa kawaida
#Akina mama lishe, machinga wasibughudhiwe katika maeneo yao
#Watengenezeeni mazingira mazuri ya watu hawa kufanya biashara katika maeneo yao.
#Tujenge mazingira ya kuwasaidia maskini hawa kufanya kazi zao vizuri.
#Ninaitaka Tz ambapo maskini anakuwa na haki sawa na matajiri...sote tumeumbwa na Mungu mmoja
#Endeleeni kumtanguliza Mungu na tuilinde amani yetu.
#Tunataka kulifanya jiji la Dar Es Salaam liwe jiji la kibiashara ndio maana sisi tumeamua kupisha kwenda Dodoma
#Nataka kuwahakikishia kuwa viwanda vinakuja...ajira zitapatikana hasa kwa watanzania wanyonge.
#Tunataka tujenge reli. Vijana mkatafute kazi kule reli inakopita...
#Mwezi ujao ndege mbili zinaingia nchini.
#Tutaboresha na viwanja vya ndege.
#Maji Dar Es Salaam yatakuwa ya uhakika.
#Afya: Tunataka kila mtanzania akienda hospitali apate dawa. Hiyo ndio Tz mpya ninayoitaka...nimecaguliwa na maskini lazima niendane nao.
#WanaCCM tembeeni vifua mbele...mambo yatakuwa mazuri tu.
#Ndio maana nataka niyafuatilie haya mafisadi yaliyobaki ndani ya CCM...mengine tayri yalisha kimbia.
#Mapato: mfano mapato ya majengo ya UVCCM, UWT, WAZAZI yanakwenda wapi. Nitayachambua haya mpaka kieleweke...nitalala nao mbele.
#Inawezekana kuja kwangu ndani ya CCM wengine hawatafurahi...lakini tutajenga upya chama chetu.
#Haiwezekani kama kikubwa hiki, kila tukitaka kufanya uchaguzi tukaombe hela kwa matajiri. Haiwezekani.
#Nataka chama kilicho okoka... Nataka CCM iendelee kutawala milele.
#Kwanini chama kikubwa hiki kama CCM hakina hata TV yake?
#Nataka CCM yenye lengo la kutawala na wala sio CCM yenye kubembeleza kutawala.
#Watanzania hasa vijana, ilifika mahali wakapoteza matumaini kwa kutawala. Tutafufua mtumaini ya vijana.
#Kuna wengine wanasema kuhamia Dodoma haiwezekani. Mbele ya Magufuli itawezekana.
#Nilishasema ndani ya miaka minne na miezi minne iliyobaki, Serikali yote itakuwa imehamia Dodoma.
#Kuhamia Dodoma hakuna mjadala.
#Mh Kinana nakupongeza sana. Umekijenga chama. Nitaendelea kujifunza kutoka kwako.
#Ninamshukuru sana Mh Jakaya Mrisho Kikwete. Nitaendelea kuchote busara kutoka kwake na viongozi waliomtangulia.
No comments:
Post a Comment