Friday, 8 May 2020

BREAKING NEWS UTUMISHI WAMWAGA NAFASI KIBAO ZA AJIRA KWA WATANZANIA*


🇹🇿 *Wanahitajika wafuatao*

▪️Ma Afisa Kilimo
▪️Ma Afisa UTUMISHI
▪️ICT Officers
▪️Wahudumu wa Afya
▪️Wahudumu wa Mochwari
▪️Washauri na Saha
▪️Watunza kumbukumbu
▪️Tutors
▪️Madaktari wa Meno
▪️Telephone operators
▪️Mafundi Bomba
▪️Wahasibu
▪️Ma Afisa Misitu
▪️Ma Afisa wanyamapori
▪️Ma Afisa uvuvi
▪️Ma Afisa Nyuki
▪️Ma Afisa Utalii
▪️Wataalamu wa maabara
▪️Ma Afisa Takwimu
▪️Mafundi Magari
▪️Ma Afisa habari
▪️Ma Engineer
▪️Insurance officers
▪️Watendaji wa Vijiji
▪️Na Nyinginezo

🇹🇿 *Maombi yote yanatumwa online kwa mfumo wa Ajiraportal*

👁️ *Deadline 21 May 2020 Bofya link hii hapa Kuanza kutuma Maombi kwa Ajiraportal*👉👉👉👉👉👉https://t.co/qIFrbBULYk?amp=1



*Usiwe Mchoyo Share Nafasi Hizi za Kazi Kwa watanzania wanaotafuta kazi*

*Sharing is caring*

🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏

Monday, 5 February 2018

WATUMISHI WASIYOIUNGA MKONO CCM KUFUKUZWA KAZI


Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amefunguka na kuwataka watumishi mbalimbali mkoani kwake ambao hawaiungi mkono Serikali ya awamu ya tano iliyopo chini ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuondoka mapema katika nafasi zao hizo.
Mnyeti amesema kuwa siku zote Chama Cha Mapinduzi ndiyo kimekuwa kikihangaika kuomba kura majukwaani huku viongozi mbalimbali wa chama hicho wakiwa si wanufaika wakubwa kulinganisha na watumishi, hivyo watumishi wanapaswa kutambua na kuiunga mkono Serikali ya CCM na kama hataki waondoke kwenye nafasi hizo. 

"Wanaoumia kuomba kura majukwaani ni CCM anayekuja kula ugali na familia yake ni wewe mtumishi, unanufaika wewe na familia yako. Sasa tumejipanga vizuri wale wote ambao siyo wenzetu watupishe mapema kabla ya uchaguzi, mimi ndiyo Mkuu wa Mkoa huu wa Manyara nasema hivi kama wewe huungi mkono Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ondoka mapema" alisisitiza Mnyeti

Sunday, 4 February 2018

Agizo elimu bure wananchi waelimishwe zaidi

Dar/Mikoani. Wakati suala la chakula likionekana kuwa tatizo kubwa katika utekelezaji wa agizo la kufuta michango, wazazi 123 mjini Tabora wamegawana fedha walizokuwa wamechangia kwa ajili ya huduma za shule na wanafunzi.
Utoaji wa elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi sekondari, ni moja kati ya mambo yaliyo katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 na Rais John Magufuli ameanza kuitekeleza kwa kupiga marufuku michango ya aina yoyote shuleni.
Kama haitoshi, Rais alirudia agizo lake Januari 17 alipotoa onyo kuwa endapo atasikia tena wazazi wakilalamikia michango, mkurugenzi wa wilaya husika ajifute kazi.
Serikali inatoa Sh23.8bilioni kila mwezi kwa ajili ya kuwezesha utoaji wa elimu bila malipo, lakini utekelezaji wa agizo hilo unakosolewa kutokana na umuhimu wa chakula kwa shule za kutwa, hasa kutokana na ukweli kuwa baadhi ya wanafunzi wanaishi mbali na shule
Uzoefu unaonyesha katika shule za nje ya miji, wanafunzi hutakiwa kufika saa 1:30 asubuhi ili kuanza masomo saa 2:00 asubuhi na hupumzika mchana kwa ajili ya chakula, lakini sasa inabidi vipindi viishe saa 8:30 mchana.
“Dhamira ya Rais ni njema, lakini fedha inayopelekwa haiwezi kutosheleza mahitaji yote,” alisema aliyekuwa ofisa elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda.
“Kwa mfano nakumbuka kuna shule moja pale Buguruni ilikuwa na wanafunzi 124 na ilipokea Sh67,000 tu ambazo hazikutosheleza. Suala la ulinzi, umeme na chakula ni changamoto katika shule nyingi.
“Serikali ikiunganisha huduma hizo kwa kuongeza bajeti, michango haitakuwa na ulazima.”
Changamoto ni chakula
Alisema athari zinazoweza kujitokeza endapo michango yote itafutwa ni pamoja na wanafunzi wengi kutofanya vizuri katika masomo yao kutokana na ukosefu wa chakula.
Maoni kama hayo yalitolewa na Profesa Benson Bana wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambaye alielezea umuhimu wa walimu kushiriki kikamilifu katika elimu ya watoto wao, kama kutoa michango ya msingi ya chakula, maji, ulinzi hata ujenzi wa miundombinu.
Profesa Bana alisema wazazi wakisitisha kuchanga kwa sababu ya agizo la elimu bila malipo, kunaweza kukawa na madhara kwa sababu ni ukweli usiopingika kwamba afya ya mwili huenda sambamba na afya nzuri ya mwili.
“Kwa uzoefu wangu wa kufundisha shule za msingi, lazima elimu iwe shirikishi kwa maana ya wazazi kuchangia ni vigumu kumuelewesha mtoto aliye na njaa,” alisema Profesa Bana.
“Wanaomshauri Rais Magufuli waangalie masuala ya msingi yanayoweza kuchangiwa na wazazi, hasa chakula shuleni.”
Alisema msingi wa elimu ya kujitegemea lazima uende sambamba na jamii husika kuchangia elimu bila wasiwasi.
“Kama walimu wanahofiwa kupokea michango, kamati za shule ziunde kamati ndogo za kupokea michango ili huduma muhimu kwa watoto ziendelee. Huwezi kuacha watoto na njaa wakati wazazi walikuwa wanachangia na wana uwezo huo,” alisisitiza.
Mtaalamu mwingine aliyezungumzia suala hilo ni mratibu wa Mradi wa Mtoto Mwerevu kutoka Jukwaa la Lishe Tanzania (Panita), Ruth Maziku aliyesema ipo hatari ya kushuka kwa kiwango cha elimu iwapo wanafunzi hawatapata chakula.
Alisema katika umri wa miaka mitano hadi 14 ambao mwanafunzi anatarajia awe kati ya darasa la kwanza na la saba, chakula ndio msingi mkubwa wa kukuza ufaulu.
“Kwa umri huo anapaswa kula milo mitano, mitatu ikiwa mikubwa na miwili midogo. Chakula kinasaidia ubongo kufanya kazi yake ipasavyo na kuongeza uelewa kwenye masomo,” alisema.
Mtaalamu huyo alisema ukosefu wa chakula unaweza kuongeza utoro kwa wanafunzi wanaoishi mbali na shule.
“Kwa hiyo wataalamu wa lishe tunasisitiza watoto kupata chakula cha mchana shuleni,” alisema.
Viongozi wa mikoa, wilaya wanena
Mkoani Iringa, mkuu wa mkoa, Amina Masenza alisema Serikali haijapiga marufuku michango ya wazazi kwa ajili ya maendeleo ya shule, bali inayokusanywa na walimu.
Masenza alitoa kauli hiyo jana alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa shule mpya ya sekondari katika kata za Nyanzwa na Ibumu Wilaya ya Kilolo.
“Ni marufuku michango yote inayotolewa na wanafunzi kwa walimu. Mwalimu atakayebainika kuhusika na hatua kali zitachukuliwa dhidi yake. Wanafunzi wanatakiwa kupokewa shuleni na kuendelea na masomo bila ya kusumbuliwa,” alisema Masenza.
“Kama wananchi mtakaa wenyewe na kukubaliana kuwa mnachanga kwa ajili ya maendeleo ya shule zenu bila ya kuhusisha mwalimu katika michango hiyo, hapo mnaruhusiwa. Hata waraka wa elimu bila malipo unasema hivyo.”
Masenza alitoa ufafanuzi huo baada ya kuulizwa maswali na baadhi ya wakazi wa Kata ya Ibumu waliotaka kujua aina ya michango iliyopigwa marufuku na ile inayoruhusiwa.
Katika majibu yake, alisema michango inayoibuliwa na jamii haina budi kusimamiwa na jamii husika bila kuwahusisha walimu, kuanzia ukusanyaji wa michango hadi matumizi yake.
Kuhusu malipo ya walinzi, mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli alisema suala la ulinzi wa shule, halmashauri yake inalipa mishahara yao katika shule zote za wilaya hiyo.
“Kuhusu usafi huo ni wajibu wa wanafunzi, na chakula tunatoa kwa wanafunzi wa bweni tu, chakula cha nini kwa mwanafunzi wa kutwa,” alihoji.
Naye katibu tawala wa Wilaya ya Kilombero, Robert Selasela alisema utaratibu wa michango ya ulinzi na chakula vinatekelezwa katika serikali ya kijiji.
Kuhusu mwongozo wa elimu bila malipo, Selasela alisema licha ya maelekezo ya fedha kujikita katika vifaa vya ufundishaji, ukarabati wa shule, huduma za kiutawala na mengineyo, bado wanavijiji wameamua kuchangia mahitaji ya chakula bila kushirikisha uongozi wa shule.
“Shule ni mali ya serikali ya kijiji. Rais anatukumbusha tu, ruzuku tuliyopata hadi Novemba mwaka jana ilikuwa ni Sh285.9 milioni, sawa na asilimia 73 ya Sh440 milioni. Bajeti ni Sh20,000 kwa kila mwanafunzi,” alisema.
“Kuhusu michango ya chakula ni wanakijiji wanakusanya chakula, si pesa na wanatumia kamati zao na kupika wenyewe.”
Katibu Tawala wa Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, Zuwena Omary alisema licha ya michango kupigwa marufuku, jamii inapaswa kutambua majukumu ya wazazi na Serikali katika suala la elimu bure.
Alisema suala la wazazi na walezi kuchangia shule za msingi na sekondari za kata ambazo wanafunzi wanaishi kwenye hosteli halikwepeki.
Wazazi walivyogawana michango
Mkoani Tabora wazazi 123 wa watoto wanaosoma Shule ya Msingi Ipuli , wamegawana fedha taslimu na vyakula walivyonunua kwa ajili ya mlo wa mchana, ikiwa ni kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais la kuzuia michango shuleni.
Makamu mwenyekiti wa kamati ya wazazi wa shule hiyo, Samson Gabriel alisema uamuzi wa kuwarejeshea wazazi hao michango hiyo ya chakula na fedha ni utekelezaji wa agizo la Rais na maelekezo ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako.
Kwa mujibu wa mwalimu mkuu wa shule hiyo, Mariam Hamis wazazi hao walichanga Sh676,000 mpaka kufikia Januari 17 na Sh272,000 zilikuwa zimetumika kununua mahindi na mchele.
“Baada ya agizo la Serikali, wazazi wameamua kugawana Sh404,000 zilizosalia pamoja na chakula kilichokuwa kimenunuliwa ambacho ni mahindi na mchele,” alisema Mariam.
Mmoja wa wazazi walioshiriki kugawana fedha na vyakula hivyo, Perpetua Kamiliwe , ambaye alikuwa ameshika kiroba cha mchele, alisema mambo yalikuwa mazuri.
“Nimechukua mchele wenye thamani ya pesa niliyochangia. Sioni kama kuna jambo limeharibika,” alisema.
Mzazi mwingine, Ibrahim Zuberi aliliambia Mwananchi kuwa licha ya kugawana chakula hicho, wanaishukuru Serikali kwa kupiga marufuku michango katika shule za umma, kwa maelezo kuwa umewapunguzia wazazi gharama na ugumu wa maisha.
“Michango hii imekuwa kero na mzigo kwa wazazi tunamshukuru Rais Magufuli kwa uamuzi wake wa busara. Hakika huyu ndiye kiongozi anayewajali wanyonge,” alisema.
“Michango ilikuwa ya viwango tofauti kati ya Sh6,000 hadi Sh10,000 kwa kila mwanafunzi.”
Hata hivyo, mmoja wanafunzi wa shule hiyo, Salome Yohana alisema uamuzi wa wazazi kutochangishana fedha kwa ajili ya chakula, utawaathiri katika masomo.
Imeandikwa na Robert Kakwesi (Tabora), Geofrey Nyang’oro (Iringa), Kelvin Matandiko na Tumaini Msowoya (Dar)     

Tuesday, 30 January 2018

Breaking news:MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2017/2018 YAMETOKA


BARAZA la Mitihani la Taifa (NECTA), latangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2017, ambapo ufaulu umepanda kwa asilimia 7.22 huku watahiniwa 265 wakifutiwa matokeo kwa udanganyifu.
Orodha ya Shule 10 Bora.
1. St. Francis Girls – Mbeya
2. Feza Boys – Dar es Salaam
3. Kemoboya – Kagera
4. Bethel Sabs Girls – Iringa
5. Anwarite Girls – Kilimanjaro
6. Marian Girls – Pwani
7. Canossa – Dar
8. Feza Girls – Dar
9. Marian Boys – Pwani
10. Shamsiye Boys – Dar
Shule Kumi (10) Za Mwisho Kitaifa
1. Kusini – Kusini Unguja
2. Pwani Mchangani – Kaskazini Unguja
3. Mwenge SMZ – Mjini Magharibi
4. Langoni – Mjini Magharibi
5. Furaha – Dar
6. Mbesa – Ruvuma
7. Kabugaro – Kagera
8. Chokocho- Kusini Pemba
9. Nyeburu – Dar
10. Mtule – Kusini Unguja
KUANGALIA MATOKEO YOTE BONYEZA LINK HAPA CHINI

Link 1: MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2017

Link 1: MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2017

Link 2: MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2017

Link 2: MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2017

           AU 
INGIA www.necta.go.tz/results/form four2017

Tuesday, 23 January 2018

SERIKALU YA TANZANIA YAAHIDI KUANZA KUBORESHA MASLAHI YA WATUMISHI BAADA YA KUMALIZA UHAKIKI 2018


Serikali ya Tanzania imeahidi kuanza kuboresha maslahi ya watumishi ya walimu ikiwemo mishahara yao kipindi hiki kutokana na kumaliza zoezi la muda mfupi la uhakiki wa wafanyakazi hewa katika sehemu mbalimbali za ajira.
Hayo yamewekwa wazi na Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe George Joseph kakunda leo (Jumatano) katika mkutano wa 10 kikao cha saba cha Bunge kinachoendelea mjini Dodoma wakati alipokuwa akijibu swali la nyongeza kutoka kwa Mbunge wa Karagwe Innocent Bashungwa alipotaka kujua ni lini serikali itawapandishia mishahara walimu.
"Utaratibu huu ambao ulikuwa umesimama kwa kipindi kifupi cha miaka kama miwili hivi kupisha uhakiki wa watumishi ambapo ni zoezi lililofanywa kwa umahiri na ueledi mkubwa, baada ya kuwa tumelikamilisha sasa tutaingia kwenye awamu ambayo ni ya kuboresha maslahi ya watumishi ikiwemo mishahara yao", amesema Mhe Kakunda.
Kwa upande mwingine, Mhe kakunda amewatoa hofu walimu wote ambao hawakupandishwa madaraja yao kutokea mwaka 2016 hadi 2017 na kudai katika mwaka huu wa fedha wameshafanya matayarisho wa kupandisha madaraja hayo. Serikali yatangaza kuboresha viwango vya mishahara kwa watumishi.
  

Sunday, 14 January 2018

UVIMBE KATIKA SEHEMU ZA SIRI ZA MWANAUME (SCROTAL MASSES)


Na Archandramu Mbungu.

Uvimbe katika sehemu za siri za mwanaume unaweza kusababishwa na matatizo mengi, mfano maambukizi katika kiwanda cha kuzalishia mbegu za kiume, Ngiri au Hernia, kuvimba kwa mishipa ya damu, kujaa maji au busha, kuvimba kwa mirija ya mbegu za kiume, saratani ya korodani, maambukizi sugu ya korodani, kujinyonga kwa korodani na matatizo mengine.
JINSI MATATIZO HAYA YANAVYOTOKEA
Maambukizi katika vifuko vya kutunzia mbegu au kiwanda cha mbegu na maambukizi sugu ya njia ya mkojo au maambukizi ya tezi dume hasa endapo mwanaume atakuwa ameshawahi kuumwa ugonjwa wa kisonono au gono ambao dalili zake ni kutokwa na usaha katika njia ya mkojo.
Wengine hupatwa na tatizo hili baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa tezi dume au endapo mgonjwa atakuwa aliwekewa mrija wa mkojo kwa muda mrefu. Ugonjwa wa kifua kikuu pia huchangia tatizo hili kwa kiasi kikubwa.
Tatizo huanza ghafla, huambatana na homa na kutetemeka na maumivu makali ya korodani, ukipapasa kwa ndani ya korodani utagusa vivimbe kama goroli kwa ndani zaidi juu ya korodani. Ugonjwa unaweza tu kutulia baada ya kuanza matibabu lakini madhara yake ni kuziba kwa njia ya kupitishia mbegu hivyo kukufanya uwe mgumba.
Maambukizi ya korodani yote huwa makali na huanza ghafla au kwa kipindi kifupi, hutokea zaidi katika kipindi cha ujana na husababishwa na maambukizi mengine yoyote ya korodani. Mgonjwa hulalamika homa kwa vipindi, maumivu ya korodani na kuvimba upande ambao una maumivu.
Hali hii ikiendelea bila jitihada za haraka kuchukuliwa, korodani hiyo husinyaa na kupotea kabisa na kukufanya uwe na korodani moja, endapo tatizo litakuwa kwenye pande zote mbili, basi korodani zote mbili zinaweza kusinyaa na kupotea na kujikuta huna korodani.
Endapo korodani itajinyonga basi itakufa kwa kutokuwepo na mzunguko wa damu wa kutosha na tiba yake ni upasuaji na kuiondoa.
Mwanaume ambaye ana korodani moja, ni vema akapime mbegu za uzazi kuona kama zipo za kutosha na yule ambaye hana kabisa korodani, uwezekano wa kuzaa haupo. Saratani ya korodani huzalisha uvimbe ambao ni mgumu kwenye korodani na hauna maumivu. Kwa hiyo, endapo una uvimbe mgumu kwenye korodani na hauna maumivu, ni vema uondolewe kwa upasuaji.
Ugonjwa wa ngiri au hernia hutokana na uwepo wa uwazi toka juu tumboni hadi ndani ya mfuko wa korodani. Njia hii huwa inakuwepo unapozaliwa na kuziba taratibu kutokana na kuendelea kwa misuli.
Kama njia ya ngiri itaendelea, husababisha matumbo kuingia humo na kujaa kwenye mfuko wa korodani. Ugonjwa huu wa ngiri ni tofauti na busha. Busha ni hali ya kujaa maji katika mfuko wa korodani na husababishwa na maambukizo ya vimelea viitwavyo filaria na huenezwa na mbu.
Ugonjwa wa ngiri pia huwatokea watoto, vijana na watu wazima. Ugonjwa wa busha na ngiri hutibika kwa upasuaji. Kinga ya mabusha ni matumizi ya dawa za kinga ya mabusha na matende ambayo kila mwaka hutolewa bure na serikali kwa wananchi wote, huwa kunakuwa na kampeni maalumu.
Ugonjwa wa ngiri hutokana na kasoro katika njia zake, ili kuepuka ni kutofanya kazi ngumu kama utagundulika una tatizo hilo.
USHAURI
Matatizo haya ya korodani husababisha matatizo makubwa ya uzazi kwa mwanaume kwa hiyo ni vizuri kuwahi hospitali kama una matatizo sehemu hiyo, usipuuze hata maumivu kidogo kwani athari zake ni kubwa.
Matatizo au maambukizi katika njia ya mkojo pia ni shida kubwa kwa mwanaume. Epuka kuumia korodani, joto kali kwenye korodani, uvutaji wa sigara, bangi na matumizi mengine ya madawa ya kulevya.
Epuka ngono zembe, vyote hivi huhatarisha afya yako ya uzazi.

Kwa mawasiliano zaidi.
Piga namba 0766245554 au 0658245554
Email:mbunguarchandramu@gmail.com

Saturday, 13 January 2018

RAIS MAGUFULI ASIKITISHWA NA MJADALA JUU YA KUONGEZWA KWA MUDA WA URAIS

Rais Magufuli ameyasema hayo leo alipokutana na Katibu mwenezi wa CCM ndugu Polepole. Zaidi soma taarifa hii kutoka ikulu