Msongo wa Mawazo au Stress kama wengi walivyozoea ni kitu kinampata kila mtu, na wakati mwingine hujui kama unastress, wapo wanaodhani mtu akiwa na stress lazima awe kama kachanganyikiwa ama analia hivi na vitu kama hivyo, wapo walio na stress na huwezi wajua na unaweza ukawa na stress usijue ukadhani ni hali yako ya mwili kawaida ila kama una dalili zifwatazo kuna uwezekano unasumbuliwa na msongo wa mawazo na haujui.
Maumivu ya kichwa ya Mara kwa MaraKama haujafanya kazi ngumu, unakunywa maji vizuri, hauna malaria wala ugonjwa wowote,hufanyi kazi juani na unapata maumivu ya kichwa mara kwa mara, hizo zinaweza kuwa stress, unatakiwa kukaa chini na kujaribu kutafuta ni mambo au kitu gani kinakupa hizo stress na ujue jinsi ya kujitoa katika msongo huo wa mawazo. Maumivu yakizidi unashauriwa kumuona daktari
Mzio au Allergies Sio kila wakati chakula Fulani Fulani, hakikupendi au mafuta Fulani unayotumia katika ngozi yako hayakupendi, si wakati wote, mzio unahusisha mazingira yako yanayokuzunguka wakati mwingine ni sababu ya stess ulizonazo, na wakati wa kukutana na wataalamu (specialist) ambazo wanaweza kukusaidia tatizo lako kwa undani.
Kujihisi Mgonjwa Mgonjwa Wakati woteUnapokuwa unajihisi homa za mara kwa mara, kuchoka sana wakati mwingine, inaweza kuwa ni dalili za msongo wa mawazo na sio tu kuwa na afya mbovu lakini pia stress zinaweza chelewesha uponaji wa kidonda chochote mwilini kama uliumia, na hii inaweza sababisha maradhi mengine kwenye kidonda chako,(infections)
Huwezi kufikiria sawasawaUnashindwa kuwaza vitu kwa umakini na kuvichanganua kwa wakati, kila kitu kinaonekana kizito hata kama ni kitu kidogo kukitafakari lakini utachukua muda kuwaza na kuwazua hii pia ni dalili ya kuwa na msongo wa mawazo (Stress) na hii huambatana na tatizo la kusahau sahau mambo.
Unakosa UsingiziKuna watu wanatumia pombe ili walale na kuna wakati wanadhani ni kawaida tu hawawezi kulala kama hawajatumia pombe, lakini kama unapata tatizo la usingizi hiyo pia ni dalili kubwa za msongo wa mawazo cha msingi ni kupunguza vinywaji vilivyo na kafaini na kufanya sana mazoezi hiyo inaweza kuufanya mwili uka relax ukapumzika vizuri lakini pia unaweza kumuona dakatri kwa ushauri zaidi juu ya afya yako.
Ni mimi Archandramu Mbungu.
Mwanasaikolojia
Mtoa Ushauri Nasaha
Kwa mawasiliano
Piga +255766245554
+255658245554

No comments:
Post a Comment